![]() |
| Sara Ibrahim, Mama wa mtoto |
![]() |
| Twaha Mussa, Baba wa mtoto |
![]() |
| Wodi ya wazazi, Mwananyamala |
Mwili wa mtoto mchanga aliyezaliwa jana katika Hospitali ya Mwananyamala ya jijini Dar es Salaam umepotea katika mazingira ya kutatanisha na kifanya hospitali hiyo kuingia katika kashfa nyingine.
Ndugu wa mzazi wa kichanga hicho Bi Sara Ibrahim amesema ndugu yao alifika hospitalini hapo tarehe 21 saa tatu asubuhi na kujifungua nusu saa baadae ambapo mtoto huyo ajulikani alipo mpaka sasa.
Ndugu mwingine aliejitambulisha kwa jina la Salmin amesema alifika hospitalini hapo majira ya asubuhi kuomba mwili wa kichanga kilichozaliwa na hupata majibu yasiyoridhisha kutoka katika uongozi huo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Charles Kenyela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema uchunguzi juu ya tulio hilo unaenelea



No comments:
Post a Comment