![]() |
| Kamanda Kova akionesha silaa zilizokamatwa |
![]() |
| Kamanda Kova akionesha pesa bandia zilizokamatwa |
![]() |
| Kamanda Kova akionesha pesa bandia zilizokamatwa |
Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa zaidi ya 51 kwa makosa mbalimbali likiwemo la wizi wa fedha katika mashine ya ATM za benki mbalimbali nchini.
Miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Raia wa kigeni aliyejulikana kwa jina la Goce au Pendarowsk aliyehusika na wizi wa zaidi ya shilingi milioni 100.
Aidha jeshi lapolisi limefanikiwa kukamata Dola za kimarekani bandia zenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 35 pamoja fedha bandia za kitanzania zaidi ya milioni 1 zikiwemo nyenzo zilizotumika kutengeneza fedha hizo.
Pia katika operation nyingine jeshi la pilisi limefanikiwa kukamata magari 18 yaliyoibiwa jijini Dar es salaam mengine yalikamatwa nje ya mikoa ya Dar es salaam likiwemo la aliyekuwa katibu Mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Fredrick Mwakalebela, na hapa analishukuru jeshi hilo kwa jitihada lililoonyesha.




No comments:
Post a Comment