Chama Cha walimu Tanzania CWT kimelaani taarifa za upotoshwaji kuhusiana na mgogoro baina yao na serikali huku kikisisitiza kuwa hakitaanza mgomo hadi pale siku zilizoombwa kuongezwa na kamati ya usuluhishi kumalizika.
Gracian Mukoba ni Rais wa CWT amezungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa bado wamekuwa wakiona umuhimu wa walimu nchini hivyo serikali haina budi kusikiliza kilio chao.
Chama hicho awali kiliweka bayana nia yake ya kuanza mgomo endapo serikali isingetimiza madai yake ya msingi. CWT pia imekanusha taarifa za kuwepo mgomo eneo lolote la Tanzania huku ikisisitiza kuwa hadi sasa umma na walimu watambue kuwa hawaruhusiwi kugoma wala kushawishi kuwepo kwa mgomo miongoni mwa walimu nchini.

No comments:
Post a Comment