Baadhi ya wateja wa benki ya NMB wameendelea kujipatia zawadi mbalimbali ikiwemo Tani moja ya mifuko ya Cement pamoja na Mabati kupitia bahati nasibu inayoendeshwa na benki hiyo ijulikanayo kama Jenga Maisha Bora.
Akiongea wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Imani Kajula amesema kuwa wameamua kuanzisha bahati nasibu hiyo ili kuwajengea wananchi tabia ya kujiwekea akiba.
Baadhi ya wateja walioibuka na ushindi huo wamewataka wananchi kuachana na tabia ya kuweka fedha katika majumba yao na badala yake wapende kujiwekea akiba za fedha zao katika mabenki.
Jumla ya wateja watano wameibuka na ushindi huo akiwemo Richard makala, Edgar Mandera, Zariah Sarungi na Ramadhan Mgunya wakazi wa jiji la Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment